I made this widget at MyFlashFetish.com.

Friday, November 26, 2010

THIS IS TIMAMU.MWANZO MWISHO


Yes...........habari zenu wapenzi wa blog hii.najua tumekua pamoja sana kwakipindi kilefu pia.msione tumekua kimya sana coz mambo ni mengi sana namajukumu ya kikazi yanachangia hasa kutowapatia habari habari kwenye mtandao huu.lakini tunawaahidi kua tuna malizi mipango ya studio ya TIMAMU RECORDS then kama kawa pande hizi.thanx 4 ma.people.by ISIAKA MC AND FURAHA.

Tuesday, November 16, 2010

LINDER MWENYE SWAGGA ZA MBELE MBELE


Ebwana kuna wanadada mbali mbali ambao ukiwaona uwa unadata live machoni kwako hasa kwa mitindo ambayo wamekua wakizolea uspuni mkubwa na umaharufu katika mitaa yao na hata sehemu nyingine.Okey uyu anaitwa LINDER.mpango mzima kama unavyomuona amepozi kwa style flani ambayo daaaa!!!!!!hatar xana.

Friday, October 15, 2010

SASA NI DA.STAMINA MKWANJA


Jamani yapo makundi mengi sana lakini kundi hili la DA.STAMINA du!!!! nishai.ok kundi hili lipo bongo dsm....mitaaa ILALA BOMA MCHIKICHI ambalo linashugulika na kzi za mziki kiujumla miyongoni mwao kati ya wasanii wanao wakilisha kundi hlo ni SHETA ,DVD THE DON,BELLE.9 nawashkaji kibao.kwasasa wanategemea kutoa tishat kali ambazo simuda mlefu ntakujuza 2 amesema hayo meneja wa kundi hilo ABUU KISAUTI a.k.a SHABAA

Friday, October 8, 2010

YEAH....UYU NDIO LILYONCE. AJA NA TOTO SHOP CLASSIC


Wanawake wengi sana skuizi wamekua wakijishuhulisha na vitu mbali mbali ilimladi kuweka maisha mzuri ya mbeleni uko tunapoelekea.uyu anaitwa LILIAN EDWIN a.k.a LILYONCE ni mama wa ntoto mmoja aneitwa KHALIFA ISIAKA ZAYUMBA a.k.a DADY.ok LILY ambae kwasasa yupo katika kazi ya uwalimu mkoani IRINGA.pia anafundisha katika shule ua kiislam ya MUSALAAM iliyopo iringa maeneo ya gangilonga.kwasasa anategemea kufungua duka la vifaa vya shule ambalo litaweza kuwasaidia wanafunzi kupata mahitaji yao kwahalaka zaidi.

Monday, October 4, 2010

PRODUCER WA VIDEO ANAECHIPUKIA


Kwasasa kumekua na ushindani mkubwa sana kwenye maswala ya utengenezaji wa vidio apa nchin TANZANIA.OK uyu jamaa anajishugulisha na utengenezaji wa video mbali mbali na ameamua kuweka maskani yake pande za IRINGA TOWN.anajulikana kama SAM.so kama vp mcheki hewan o759288441

Sunday, October 3, 2010

UYU NDIO FURAHA WA TIMAMU RECORD'S


ebwanaaaaaaaa! huyu ni firstlady kutoka TIMAMU RECORD's anaye fanya vizuri katika mziki wa kizazi kipya nchini TANZANIA.
hivi sasa TIMAMU inavituvingi vya kufanya kuhakikisha project za studio na za intertainment kwa ujumla zina kwenda sawa.
kama humjui huyu anaitwa; "FURAHA" amesha achia kazi yake ambayo amemshirikisha LINEX na ANNET inayo kwenda kwa jina la MAPIGO YA MOYO, na siyo muda mrefu ataachia kaziyake mpya itakayo kwenda kwa jina la " MZIKI KAZI" ambapo humo ndani amemshirikisha NEMO......

PRODUCER TC WA 69 RECORDS SASA AJIPANGA UPYA


Mchizi uwa anakubalika sana katika kufanya kazi zake za uzarishaji wa mziki nchini TANZANI.anajulikana kama TC.ya kwakipindi kilefu amekua kimya coz mchizi alikua anaongeza ujuzi wake katika chuo cha sanaa bagamoyo.OK amesema soon watu watapata kusikia kazi zake upyaaaaaaaaaaaaa.

AKIWA STUDIO KATIKA KUTENGENEZA BEAT

YASINTA......... AMERUDI KUTOKA CHINA.....SASA MMMH.....PANDE ZA SINGAPOL


Jamani kweli life is change.mmmh!!!!Uyu anaitwa YASINTA kwakipindi kirefu ayupo bongo alisanukia pande za SINGAPOL uko kutafuta life. kurekebisha mpango mzima wa home.Yes....na kwenye michezo ya kitoto nimecheza nae sana yeye alikua mama na mm isiaka nilikua baba.Duuuuuuuu...jamani haya tena uyu ni mchizi wangu ile mbayaaaaaaaa.

Friday, October 1, 2010

TEMMY.G ASEMA WASANII WANAZIGUA IRINGA


Moja kati ya PRODUCER ambae anafanya vizuri mkoani IRINGA.ni TEMMY MAHONDO a.k.a TEMMY.G jamaa amesema mziki umekua ni kazi kubwa sana ambayo inaingiza mapato makubwa kwenye nchi yetu lakini kuna watu ambao wanataka kauharibu.hasa kwa sasa IRINGA wasanii wengi wamekua awana upeo mkubwa wakubwa na kufikilia nini wafanye katika game hili la BONGO FLEVA

Wednesday, September 29, 2010

JAMANI WADAU WANGU WA TIMAMU SANA. NAWAOMBA LADH SANA


Yeah....Mambo vipi? OK napenda kuchukua fulsa hii na muda huu kuwaomba ladh kwa kutowapatia habari kwa muda mrefu kidogo.nafikili majukumu yamekua mengi sana hasa ya kifamilia zaidi ndio mana nikawa nashindwa hata kutembelea uwanja wetu huu wa wa habari.OK kwsasa nimerudi tena kama kawa wazeiyaaaaaaaaaaaaa.its me ISIAKA,MC.............

DVD NA ISIAKA.MC BATA DEILEEEEEEEEE.


Teh...teh...teh.Yah.hivi ndivyo tunavyokua tukiwa kwenye matundu yetu jamaniiiiiii.

DJ.NAS VICHECHE SASA BASIIIIIIIIIIIIIII......


Duuuuuuuuuuuu!!!! Huyu nimoja kati ya maDJ wakali sana mkoani IRINGA.jamaa anaitwa NICKSON SANGA.a.k.a DJ.NAS anafanya kazi katika kituo cha radio COUNTRY FM 88.5.amekaa chini nakusema vicheche sasa basi kwamana anataka kutulia na mpenzi wake watokea zamani yani.OLESTA' nas amesema pia aoni faida yoyote kua na mdemu wengi wakati yeye anajali afya yake kiujumla.chamwisho amesema kua atoacha kupendeza kwani yeye ndio hobi yakeeeeeeeeeeeeee.....,

DJ.NAS NA MAMA WATOTO. OLESTA;

ZANDER SASA AJA NA MASHAMBULIZI KWENYE GAME


Yes,,,,Ebwana mchizi anajulikana kama ALEXANDER NGALIKA.lakini katika mpango mzima wa bongo fleva anatambulika kama ZANDER.Mchizi alianza game hili kitambo kidogo alikini katika kutafuta maisha pia kumemfanya kama achelewe kusikika redion.OK kwasasa jamaa anatamba na kazi kama 3 hivi nazo ni kama vile.SABRINA ambayo amemshikisha BERRE.9 na SIFA PEKEE ambayo pia amefanya na BARAKA,B.U.X & DOCTOR na nyingine amshikisha mwana dada kutoka timamu records ni ANET.ZANDERamesema kua ameshasoma mpango mzima wa hili game linavyokwenda kwaio watu wakae tayali kupata ladha nyingi kutoka kwake.

Thursday, June 17, 2010

KASAMPAIDA AKIWA NA ISIAKA.MC KWENYE CONSERT YA MR&MISS RUCO


Ebwana da!!!!! nishai hii ilikua noma coz watu walitiga kwenye show 9t alafu wakala sana bata.na hivi kama unavyowaona KASAMPAIDA NA ISIAKA.MC

Thursday, June 10, 2010

HUYU NDIO '''SIKWELI''' KUTOKA IRINGA TOWN


Yeah...huyu ndio mchizi anajulikana kama vile 'SIKWELI'nimsanii wa miondoko ya kizazi kipya yani BONGO FLEVA.jamaa ambae maskani yake ipo IRINGA TOWN ameamua kwasasa kufanyia plomotion ngoma yake mpya ambayo ameifanyia katika studio za REN BOW RECORDS na producer ambae ni mahili kuwatoa watu mkoani apo kimziki TEMMY.G

Thursday, April 22, 2010

SHETA KUJA NA KUNDI LA DAR,STAMINA


Ebwana daaaa!!!!dogo huyu anaitwa NURUDINI a.k.a SHETA ameamua sasakufanya kazi ya mziki rasmi coz kwamda mrefu alikua akipenda sana kufanya ili game lakini shule ndio ilikua kikwazo kwake.pia amesota sana kwenye game ili.lakini kwasasa nimuda wakumpokea kwamikono miwili.SHETA kwasasa ametoa SINGLEambayo imeanza kufanya vizuri katika radio mbali mbali nchini TANZANIA.single hiyo ameifanyia katika studio za A.M RECODRS chini ya producer MANEKE,SINGLE iyo ameipa jina la ME NA PLAY pia amemshilikisha MWANA,F.A a.k.a BINAMU

Thursday, April 15, 2010

HILI NDIO GARI LA MANENO JAMANI


Ebanaaaa da!!!!huyu ni HATIA OMARY a.k.a GARI LA MANENO,nimoja ya watangazaji ambao wamepata umaharufu mkubwa sana mkoani IRINGA,ok amekua akiwakonga sana watu nyoyo zao hasa pale anapokuwa kwenye kipindi chake cha TAHARABU ambacho kinarushwa na 87.8 EBONY FM,lakini jamani mmmh!!!!ayah.

JUMA NATURE KUFUNGUA STUDIO


JUMA KASSIM KIROBOTO.yani JUMA NATURE sasa jamaa ameamua kufungua studi ambayo itawasaidia wasanii mbali mbali ili kukamilisha mpango mzima kwenye hili game la BONGO FLEVA nchini TANZANIA,studio hiyo ameipa jina la HALISI RECORDS ambayo ipo maeneo ya mbagala mahali anapoishi mwenyewe KIROBOTO.pia studio hiyo imeshaanza kutoa kazi kama vile ya mshikaji wa MABAGA FLESH, JB ndio amekua wakwanza kuibikili studio ya HALISI RECORDS.

SASA NIKWELI Q.JAY AMEOA


Kama nilivyokuhaidi kua lazima tujuwe ukweli kuhusu mchizi Q,JAY kama ameoa.Yah hivi ndivyo mambo yalivyokua siku ya harusi yake.ok BIG UP sana mwanetu kuanza maisaha mapyaaaaaaaah.

Tuesday, April 13, 2010

Q,JAY YASEMEKANA JAMAA AMEFUNGA PINGU ZA LIFE


Hivi karibuni tumepata kusikia habari kua msanii wa kundi la WAKALI KWANZA maharufu kama Q,JAY amefunga pingu za maisha kimya kimya na bila ya watu kufahamu atujajua kwanini ameamua kufanya kimya kimya OK TIMAMU itamtafuta ili atujulishe ni kweli au la,

FERY KANO AMEAMUA KURUDI TENA DAR


Moja kati ya wasanii wazuri katika miondoko ya R&B ni FERY KANO jamaa ambae anauwezo mkubwa sana katika kuchezea voice yake kwenye uwimbaji.hivi sasa ameamua kurudi jijini D.S.M baada ya kuachana na band ya sweet noiz.ambayo alikua akifanyia kazi kwa mda mrefu iliyopo mkoani IRINGA

Thursday, April 8, 2010

MUNGU MWENYEWE NDIO ANAJUA.


Kama unavyoona uyu ndio jamaa amegongwa nagari maeneo hayo ya UBUNGO.madereva inatakiwa wawe makini sana na bara bara coz bila hivyo tutazidi kupata ajari za kila siku nchin kwetu TANZANIA.

AJARI ILIKUA NIMBAYA SANA DA!!!!!!

AJARI KUBWA AMBAYO IMETOKEA UBUNGO JUZI


niajari kubwa sana iliyotokea juzi maeneo ya UBUNGO kama unavyoona nijinsi gani majerui alivyokua amelala chini na kupoteza mwelekeo wa maisha.STORY by DIMO IMAGE PROFESSIONAL

Friday, March 26, 2010

RAINBOW RECODRS KUSAKA VIPAJI KWA KUDAKA MIC


RAINBOW RECODRS ambayo inamilikiwa na producer TEMMY.G amesema hivi karibuni anataka kuaanda tamasha la muziki wa kizazi kipya ilikusaka vipaji vya HIP HOP nchini TANZANIA natamasha hilo litapewa jina la DAKA MIC. ameyasema hayo hivi karibuni alipokua anaHojiwa na radio COUNTRY FM 88.5 iliyopo mkoani IRINGA.haya wasanii wa HIP HOP kazi kwenu sasa.

EBWANA DAAAAAAA!!!!!!!!!! HII NOMA,

Wednesday, March 24, 2010

CHIDY BEENZ TUZO KWANGU LAZIMA


RASHID ABDALLAH MAKWILO a.k.a CHIDY BEENZ ambae anawakilisha kundi zima la LA,FAMILIA ambalo kundi hilo maskani yake ni ILALA BOMA FLAT.,Yah jamaa amesema tuzo kwake nikawaida coz anaamini kipaji anacho chakutosha kwani kazi anayoifanya kwakutoa burudani kwa mashabiki wake anaamini ni babkuwa.chid nimsanii ambae anafanya miondoko ya HIP HOP nchin TANZANIA na ametokea kupendwa nawatu wa aina mbali mbali.

TANZANIA UHURU NA UMOJA


Bado tunajivunia nchi yetu ni ya amani na upendo.hii ndio nembo yetu inayotutambulisha kua sisi ni TANZANIA.wapenda amani na upendo

Monday, March 22, 2010

MY DREAMS YA FANYA VIZURI KITAANI


Uwezi amini apa kati kati zimetoka filamu nyingi sana zawasanii mbali mbali.lakini kwasasa mtaani bonge la filamu la MY DREAMS limeonekana kupenda sana hasa kama utapata kuiyona lazima utakubaliana na kazi za wasanii wa kuigiza filamu nchini TANZANIA.ndaniya MY DREAMS yupo mkali VICENT KIGOSI a.k.a REY na DK.CHENI nawakali kibao ambao wamebobea katika fani hiyo ya uwigizaji.

AMANI........ LIVE SHOW IN.....MANCHESTER


Mwana dada AMANI kutoka nchini NAIROBI KENYA anategemea kufanya bonge la show siku ya tarehe 03/04/2010 ndani ya MANCHESTER

MANEKE AKIWA ANANYONGA BEAT STUDIO


Wasanii wamekua wakimkubali kazi zake ambazo amekua akitoa.napia MANEKE awali alishawai kufanya kazi na studio kama vile MID MAN RECODRS,DHAHABU RECODRS, BAUCHA RECODRS na nyingine nyingi.lakini kwasasa yupo ndani ya A.M RECODRS.

PRODUCER MANEKE NDANI YA ......A.M RECODRS


Bwana mdogo ambae kwasasa amekua gumzo kwenye utayarishaji wa mziki wa BONGO FLEVA.ni MANEKE na kama unavyomuona akiwa yupo katika studio za A.M RECODRS akiendelea kufanya mambo kadha wa kadha ili kuakikisha anaendelea kubaki kwenye chati ya utayarishaji wa mziki nchini TANZANIA

Friday, March 19, 2010

CAPTEN ZANGE MPANGO MZIMA NA SHAMPENI...


Uyu jama amini usiamini ni matata sana manake d!!!OK anaitwa CAPTEN ZANGE alifanya part ipendeze sana hasa watu pale walipotangaziwa kuwa sasa ni mda wa kufungua shampeni.shangwe zakutosha kutoka kwa mabinti uku CAPTEN akisamama kwakulinga.

DJ.NAS AKIMLISHA KEKI MDAFADA HUYO


Usifanye mchezoooooo,hasa ulipofikia wakati wakulishana keki ilikua kama hivi.na huyu ni DJ.NAS live bila chenga

EBWANA DA!!! WANYAMWE JUZI KATI NDANI YA PART


Uwezi amini juzi kati wanyamwezi tulialikwa kwenye B,DAY ya mwanadada mmoja ambae ana wakubali sana wanyamwezi wa apa town.ndio ivyo kama unavyotuona.uyu wa kwanza ni DJ.NAS,alafu anafwatia ISIAKA MC,uyu mwingine ni mtumzima TOJO a.k.a TJ

Thursday, March 18, 2010

MASANJA KUSHUUDIA AJARI MTO RUAHA


Mchekeshaji wa kundi la ZE,KOMEDI masanja pichani kama umuonavyo akishudia ajali ya gari iliotokea kipindi cha nyuma kidogo alipotembelea mkoani IRINGA.na kwenda kuona mto RUAHA siku iyo ilikua mvua zimenyesha sana kiasi ambacho kukuta gari limezama.

SNA LEE....SIJUI MZIKI UMEISHIA WAPI,


Ki,home home jamaa hua tuna mwita BABU ALLY lakini mashabiki wa mziki wa BONGO FLEVA wanamtambua kama SNA LEE.jamaa alijizolea umaarufu mkubwa sana kipindi cha nyuma pindi pale alipotoa singo yake iliyojulikana kama WACHA PARTY IANZE.ambayo alimshilikisha DULLY SYKES a.k.a MR,MISIFA.kiukweli atujui mbaka sasaivi uyu jamaa anafanya ishugani?????......na kama unavyomuona shavu dodo.

ISIAKA MC NA JOSLIN NI FLENDS TOKEA ENZI HIZO


Du!!! urafiki ulianza siku nyingi sana hasa ukizingatia mziki ndio ulitukutanisha na hadi kua kama ndugu.Yah nimda mrefu sana kiasi ambacho ukiambiwa unaweza kushangaa sana na kujiuliza kua du!!! kumbe hawa ni ndugu coz kwenye matatizo hua tunasaidiana sana.nawatu wengine walishawai kutaka kutugombanisha lakini imeshindikana live.ok kama unavyotuona apa ISIAKA MC na JOSLIN a.k.a MZEE wa PERFUME

Thursday, March 11, 2010

EBWANA DA!! BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LATANGAZWA


Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE ametangaza baraza jipya la mawaziri,baada ya kuvunja baraza la mawaziri kufutia EDWARD LOWASA kujiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa ya richmond

STEVEN A.K.A KASAMPAIDA NDANI YA IRINGA


Mchizi STEVEN MAGOMBEKA a.k.a KASAMPAIDA. ambae anapenda sana kujishuhurisha na kazi mbali mbali zaidi kwenye maswala ya computer. jamaa ameamua kuingia IRINGA TOWN kwahajili ya kucheki mpango mzima wa life litakwendaje kwa kufungua ofic ambayo itakua ikidill na mambo ya kubun CD,kufanya SHOOTING,na ana PLINT TISHET katika kiwango kizuri zaidi.Hayaaaaa wadau wa mkoani IRINGA kama vp fikeni KASAMPAIDA.

,,,,,,,,,,KASAMPAIDA,,,,,,,,,

.......I NEED TO MONEY OOH!!!


Kwasasa kila kitu fedha du!!!! jamani jaman cheche je???

.....JHIKO MAN IN AFRIKABISA BAND.....

Wednesday, March 10, 2010

JAY MOE KUACHIA KAZI YAKE YA SOME MONEY


JAY MOE nadhani tunamfahamu vizuri katika game hili la HIP HOP nchini TANZANIA.ok JAY MOE ameachia mzigo wake mpya ambao ameufanyia studio za FISH CRAB na pruducer LAMAAR na track iyo inakwenda kwa jina la SOME MONEY kama wiki 2 hivi ndio imeachiwa kama ujaisikia fatilia.

TIMAMU RECODRS KUJIANDAA KUTOA TISHET


Ebwana da!!!inawezekana ikawa ni muda wa TIMAMU RECODRS kufanya mapinduzi kila sekta coz hiyo unayoiyona apo juu ni logo ambayo atakua kwenye tishet ambazo tunategemea soon zitakua mtaani kwaajili ya biashara zaidi.