Friday, February 26, 2010
NASIR JONES A.K.A NAS HIP HOP REAL
Nasir Jones (amezaliwa tar. 14 Septemba, 1973) ni mwanamuziki wa rap na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake kisanii kama Nas. Zamani alikuwa akijiita Nasty Nas. Nas ni mtoto wa mwanamuziki wa jazz wa zamani Mzee Olu Dara. Alizaliwa na kukulia katika nyumba za miradi za mjini (nyumba za watu wenye kipato cha chini) Queensbridge, New York.
Nas alisaini mkataba na studio ya Columbia Records mnamo mwaka wa 1994, na kutoa albamu yake ya kwanza ya Illmatic. Albamu ya Illmatic ilipata kuwa bora na kufahamika zaidi na mauzo bora.
Baadaye albamu kadhaa za Nas zilifuata. Albamu hizo ni pamoja na It Was Written ya 1996, I Am... and Nastradamus ya 1999, na Stillmatic ya 2001. Nas alikuwa mmoja kati ya wanakundi la muziki wa rapna hip hop - The Firm, ambalo limejumlisha wasanii wengine kama vile AZ, Foxy Brown, na Nature. Ingawa, kundi halikufanya kazi nyingi na badal yake wakatoa albamu moja tu ya pamoja.
Kuanzia mwaka 2001 hadi`2005, Nas aliusishwa katika ugomvi mkubwa na rapa mwenziwe Bw. Jay-Z. Marapa wote walikuwa wakishambuliana kwa kutumia nyimbo zao.
Wawili hao ugomvi wao ukaja kwisha baada ya kualikwa katika tamsha la muziki la New York City-area hip-hop za vituo vya redio. Nas akasaini mkataba na studio ya Jay-Z maarufu kama Def Jam mnami mwaka 2006.
Albamu yake ya kwanza akiwa kama mmoja wa Def Jam, ilitoka mwaka wa 2006, ikiwa na jina la Hip Hop is Dead, ikiwa imeambatana na albamu nyingine ya mwaka wa 2008, iliyokwenda kwa jina la Untitled.[1]
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment